VIDEO: Yanga kuwafuta mashabiki machungu ya Simba leo

Muktasari:

  • Yanga inatarajiwa kucheza mchezo wake  wa 25 ikiwa na kumbukumbu ya kufungwa 1-0 na Simba mchezo uliopita kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kikosi cha Yanga kinashuka leo Jumatano kikiwa kimejipanga kuwapa raha mashabiki wake kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.

Kocha Mwinyi Zahera ameweka wazi kwamba kuna kitu kikubwa wachezaji watafanya leo kwa ajili ya mashabiki wao.

Yanga wanashuka kwenye mchezo huo  wakiwa kileleni na alama zake 58, pia wakifuatiwa na Azam FC ambao wapo nafasi ya pili wakiwa na alama 50 baada ya kupata sare ya bao 1-1 dhidi ya Coastal Union jana Jumatano.

Watani zao Simba wamejiimarisha katika nafsi ya tatu wakiwa na alama 42 baada ya kushinda mchezo wao wa jana Jumanne waipokutana na African Lyon  kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Mbao FC wapo nafasi ya 6 kwenye msimamo huo wakiwa na alama  36 wakicheza mechi 26.

Hata hivyo Yanga inacheza mchezo wake  wa 25 ikiwa na kumbukumbu ya kufungwa 1-0 na Simba mchezo uliopita kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.