VIDEO: Yanga yatambulisha wachezaji nane

Muktasari:

  • Mwenyekiti wa kamati hiyo Antony Mavunde amesema mpaka sasa michango ya wanachama na mashabiki wao imekamilisha usajili wa wachezaji nane.

KAMATI ya kukusanya michango ya Yanga imetambulisha wachezaji nane wapya waliomaliza kusajiliwa huku ikisema zoezi linaendelea.
Mwenyekiti wa kamati hiyo Antony Mavunde amesema mpaka sasa michango ya wanachama na mashabiki wao imekamilisha usajili wa wachezaji nane.
Mavunde ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu amesema mpaka sasa kamati ya usajili imefanikisha usajili huo kutokana na fedha za michango hiyo.
Mavunde amewataja wachezaji hao kuwa ni mabeki Lamine Moro(Ghana),mustapha Seleman(Burundi).
Wengine ni pamoja na washambuliaji Sadbey  Ukhob, Issa Bigirimana, Patrick  Sibomana, Juma Balinya, Kalengo Maybin na Mzanzibar Kiungo Abdulaziz Makame.
Aidha Mavunde amesema usajili bado unaendelea na wachezaji wote watatambulishwa rasmi katika kilele maalum cha wiki ya Mwananchi itakayokuwa na matukio mbalimbali.