Mastaa Marekani watumbuiza tamasha alilosusia Nick Minaj Saudi Arabia

Friday July 19 2019

 

By AFP

Janet Jackson, 50 Cent na Chris Brown ni miongoni mwa wanamuziki waliotumbuiza katika tamasha nchini Saudi Arabia ambalo rapa Nicki alijiondoa kutokana na masuala ya ukiukwaji wa haki za binadamu.
Mashabiki waliokuwa wakishangilia, walidansinyimbo zilizokuwa zikiitumbuizwa katika tamasha hilo lililopewa jina la Jeddah World Fest, lililoandaliwa katika jiji la Red Sea kusini mwa Saudi Arabia.
Taswira za tamasha hilo, ambayo isingefikirika kutokea miaka miwili iliyopita, inaonyesha ni kiasi gani taifa hilo la kihafidhina uliopiiliza linalegeza masharti ya kudhibiti burudani.
Minaj -- anayejulikana zaidi kwa mashairi yake yenye maneno makali, ya ngono na video zinazoonyesha utupu -- alijiondoa katika tamasha hilo katika kuonyesha mshikamano kwa wanawake katika taifa hilo hafidhina.
Kitendo cha kujiondoa kiliamsha mjadala kwenye mitandao ya kijamii, huku mashabiki wakieleza kukerwa na uamuzi huo na wengine wakitaka kurudishiwa fedha walizolipia tiketi.
Nyota huyo wa rap alisema katika akaunti yake ya Twitter kuwa uamuzi wake wa kujiondoa haukulenga kuonyesha kutoiheshimu serikali ya Saudi Arabia.
Vikikariri chanzo cha habari ambacho hakikuwekwa bayana, vyombo vichache vya habari, likiwemo gazeti linaloiunga mkono serikali la Okaz, vilisema ni falme hiyo iliyofuata onyesho la Minaj kwa kuwa maonyesho yake huwa na vitendo ambavyo ni kinyume na mila na utamaduni wa Saudi Arabia.
Nyota wengine wa Marekani waliotumbuiza katika tamasha hilo ni rapa Future na DJ Steve Aoki.

Advertisement