Taylor Swift aruhusiwa kutumbuiza nyimbo za zamani tuzo za American Music Award

Muktasari:

Kampuni ya kurekodi muziki aliyofanya nayo kazi katika albamu sita za kwanza imesema nyota huyo wa pop anaweza kutumia nyimbo azipendazo.

New York, Marekani. Kampuni iliyokuwa ikifanya kazi na Taylor Swift imesema jana Jumatatu kuwa inamruhusu nyota huyo wa muziki wa pop kutumbuiza baadhi ya nyimbo za mwanzoni katika tamasha la kutuza wasanii, ikiwa ni hatua mpya katika mgogoro wa takriban mwezi mmoja kuhusu haki za mwanamuziki huyo katika albamu zake sita za kwanza.
Lakini hata hatua hiyo inayoonekana kuelekea katika suluhu, haikufanyika bila ya kuibua utata.
Lebo ya The Big Machine Label Group ilitoa kile ilichokiita taarifa ya pamoja na Dick Clark Productions -- ambayo inajihusisha na tuzo za muziki za Marekani (AMA) -- ikisema wamefikia makubaliano ya kutoa leseni ambayo itamruhusu Swift kuimba nyimbo anazotaka katika tamasha hilo litakalofanyika Novemba 24.
Lakini muda mfupi baadaye, watayarishaji hao walijitenga na taarifa hiyo wakisema makubaliano ni baina ya Swift na lebo yake ya zamani.
Big Machine, ambayo ina makao yake makuu Nashville, ikafafanua baadaye kuwa "iliitaarifu" kampuni hiyo ya ikutayarisha muziki kuhusu kutoa leseni hiyo ya kumruhusu Swift kuimba nyimbo atakazo.
Msemaji wa Swift hakupatikana mara moja kuzungumzia suala hilo baada ya kuulizwa na AFP, na nyota huyo wa pop bado hajajitokeza kuzungumzia.
Wiki iliyopita, Swift -- anayejulikana kwa mahesabu yake ya matumizi ya mitandao ya kijamii -- alisema katika Tumblr kwamba viongozi wa Big Machine walikuwa wakitaka kumdhibiti kinguvu.
Alidai kuwa walimwambia "haruhusiwi "kutumbuiza nyimbo zangu za zamani katika televisheni kwa sababu hiyo itakuwa ni kurekodi upya muziki wangu kabla sijaruhusiwa mwakani".
Nyota huyo wa pop anayejulikana kwa nyimbo kama "Shake It Off" na "We Are Never Ever Getting Back Together" -- pia alisema Big Machine inamzuia kutumia nyimbo zake za zamani au vipande vya vi9deo za maponyesho yake katika mradi wa chaneli ya filamu ya mitandaoni wa Netflix.
Kampuni hiyo, ambayo haikutaja suala la Netflix katika taarifa hiyo ya jana, iloikanusha madai yao wiki iliyopita.
"Lazima ifahamike kuwa wanamuziki wanaorekodi hawahitaji ruhusa kwa ajili ya maonyesho yao yanayorushwa moja kwa moja na televisheni au aina nyingine yoyote matangao ya moja kwa moja," Big Machine ilisema jana Jumatatu.
"Ruhusa ya kampuni inayorekodi inatakiwa tu kwa wasanii walio na mikataba ya kazi zao zilizorekodiwa za audio (sauti) au visual (video) na katika kuamua kazi hizo zitasambazwaje."
Swift alianza kupambana hadharani na tajiri katika sekta hiyo, Scooter Braun kuanzia katikati ya mwaka kuhusu kununua kampuni hiyo aliyokuwa akifanya nayo kazi kwa zaidi ya miaka kumi iliyopita, hatua iliyomuwezesha kumiliki sehemu kubwa ya haki za albamu zake sita za kwanza.
Baadaye mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 29 aliahidi kurekodi upya albamu zake zxa mwanzo na kuzalisha nakala atakazokuwa anamiliki, akisema mkataba wake unemruhusu kuzifanyia nkazi upya albamu zake kuanzia ya kwanza hadi ya tano ifikapo Novemba 2020 -- muda ambao amepanga kurejea studio kufanya hilo.
Swift alisaini mkataba mpya na kampuni ya Universal Music Group mwaka 2018 ambao unampa haki ya kumiliki nakala halisi (master), kwa kuanzia ba al;bamu yake ya saba inayoitwa "Lover".