Mgonjwa wa Magufuli atoka hospitali

Tuesday March 28 2017

By Ephrahim Bahemu, Mwananchi ,[email protected]

Dar es Salaam. Neema Wambura, Mgojwa aliyekuwa anatibiwa majeraha ya moto katika Hospitali ya Taifa Mhumbili (MNH) kwa udhamini wa Rais John Magufuli, ameruhusiwa leo (jumanne) baada ya kupona vizuri.
Mara baada ya kuruhusiwa Wambura amesema sasa yupo vizuri kuweza kuendelea na maisha ya kawaida ila matamanio yake ni kufungua biashara ya duka Jijini Mwanza na hataki kurejea tena  Mkoani Mara.
"Madaktari walinipatia huduma nzuri, nimeweza kupona lakini siwezi kuishi tena mara natamani kama ningepata makazi Mwanza, nikafungua biashara ya yoyote ambayo itaniwezesha kitunza watoto wangu watatu," amesema Wambura.