Mradi wa maji kunufaisha wanavijiji 5,000

Thursday January 18 2018

By Haika Kimaro, Mwananchi

Mtwara. Zaidi ya wakazi 5,000 kutoka vijiji vya Mayaya, Mtendachi, Namindondi na Malanje kata ya Madimba, Wilaya ya Mtwara sasa wameondokana na adha ya kuamka usiku kwenda kutafuta maji.

Unafuu huo unatokana na kuzinduliwa kwa mradi wa maji katika kijiji cha Mayaya, kazi iliyofanywa na Waziri wa Maji, Mhandisi Isack Kamwelwe.