VIDEO: Wanaotumiwa kuihujumu NCU kizimbani

Thursday January 18 2018

By Jesse Mikofu, Mwananchi

 

Mwanza. Watu wawili wamepandishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi mwanza Januari 17 wakikabiliwa na mashtaka matatu ikiwemo kuhujumu mali yenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 10.073 za Chama cha Ushirika Nyanza (NCU).

Waliosemewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi mwandamizi, Gway Sumaye ni Anthonia Wambura na Timoth Kilumile, wote wakazi wa jiji la Mwanza.