Mbeya yaongoza uingizaji vipodozi bandia nchini

Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA), Gaudensia Simwanza.

Muktasari:

TFDA imeteketeza bidhaa nyingi za aina hiyo zilizoingizwa kutoka nchi za Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Zambia na Malawi.

Dar es Salaam. Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imeutaja Mkoa wa Mbeya kuongoza kwa kuwa na matukio mengi ya uingizaji bidhaa za vipodozi zisizofaa kwa mwaka 2016.

Sambamba na hilo, TFDA imeteketeza bidhaa nyingi za aina hiyo zilizoingizwa kutoka nchi za Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Zambia na Malawi.

Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa mamlaka hiyo, Gaudensia Simwanza alisema jana kuwa vipodozi katika mkoa huo huingia kupitia mpakani na njia za panya.

Habari zaidi soma Gazeti Mwananchi