Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Krismasi yaondoka na maisha ya watu Dar, K’njaro

Naibu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lucas Mkondya.

Muktasari:

Katika matukio hayo, watu watano wakiwamo wanafunzi wanne wamekufa maji jijini Dar es Salaam na Rombo, Kilimanjaro na wengine saba wameuawa na wananchi baada ya kuwatuhumu kukwapua vitu mbalimbali.

Dar/Moshi. Watu kumi na moja wameripotiwa kufariki dunia katika matukio mbalimbali wakati wa Sikukuu ya Krimasi.

 Katika matukio hayo, watu watano wakiwamo wanafunzi wanne wamekufa maji jijini Dar es Salaam na Rombo, Kilimanjaro na wengine saba wameuawa na wananchi baada ya kuwatuhumu kukwapua vitu mbalimbali.

 Jijini Dar es Salaam, wanafunzi wawili moja wa shule ya msingi na mwingine sekondari, walikufa baada ya kuzama kwenye kina kirefu cha maji wakati wakiogelea.

 Naibu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lucas Mkondya amesema watu hao walifariki dunia katika maeneo tofauti.

 Amesema mwanafunzi wa darasa la pili aliyekuwa anasoma Zanzibar, Hafidhi Bubu alikufa maji wakati akiogelea kwenye ufukwe wa Bamba Kigamboni. Mwanafunzi huyo alikuwa likizo kwa baba yake ndipo siku hiyo ya sikukuu alipokwenda kuogelea kwenye ufukwe huo.

 Siku hiyohiyo, mwanamume ambaye hajatambulika jina lake alifariki dunia baada ya kuzama kwenye kina kirefu wakati akiogelea katika eneo la Coco Beach.

Kwa habari zaidi soma gazeti la mwananchi