Live Lugola akizungumzia matukio ya utekaji

live Lugola kuzungumzia kutekwa kwa Mo Dewji

Muktasari:

Leo Jumamosi Oktoba 13, 2018 muda wowote kuanzia saa 9 alasiri  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,  Kangi Lugola anatarajiwa kuzungumzia msako wa mfanyabiashara Mohammed Dewji ‘Mo Dewji’ aliyetekwa Alhamisi Oktoba 11, 2018


Dar es Salaam. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,  Kangi Lugola leo Jumamosi Oktoba 13, 2018 muda wowote kuanzia saa 9 alasiri atazungumza na vyombo mbalimbali vya habari jijini Dar es Salaam.

Miongoni mwa mambo yanayotarajiwa kuzungumzwa na Lugola ni tukio la kutekwa kwa mfanyabiashara Mohammed Dewji ‘Mo Dewji’.

Mfanyabiashara huyo alitekwa juzi alfajiri Oktoba 11, 2018 jijini Dar es Salaam kwenye Hoteli ya Colosseum iliyopo Oysterbay alipokwenda kwa lengo la kufanya mazoezi.

Dewji ambaye miaka mitatu iliyopita jarida la Forbes lilimtaja kuwa tajiri namba moja Afrika kwa vijana walio chini ya miaka 40 alitekwa na Wazungu wawili waliomvizia alipokuwa akishuka kwenye gari lake ili aingie kwenye mazoezi kwenye gym ya Hoteli hiyo.

Taarifa za kutekwa kwa mfanyabiashara huyo anayekadiriwa kuwa na utajiri wa Sh3.5 trilioni zilianza kusambaa Alhamisi saa 1:00 asubuhi katika mitandao ya kijamii, kabla ya polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam kuthibitisha saa mbili asubuhi.