Bulaya atinga tena kituo kikuu cha polisi
Muktasari:
Bulaya amefika polisi saa 1:30 asubuhi
. Mbunge wa Bunda Mjini (Chadema), Ester Bulaya ameripoti kituo kikuu cha polisi cha Kanda Maalumu ya Dar es Salaam leo Aprili 16, 2018 saa 1:30 asubuhi akiitikia wito wa polisi.
Bulaya amesema bado hajaelezwa chochote.
"Ninaendelea kusubiri nipate maelekezo kujua kinachoendelea,” amesema.