CCM yapitisha sita Eala, Mnyaa wa CUF apenya

Spika wa Bunge, Job Ndugai 

Muktasari:

Wabunge waliopita kwa kupigiwa kura kwa upande wa CCM  ambao ni kundi A ni  Fancy Nkuhi, Happines Legiko, Maryam Ussi Yahya, Dk Abdullah Makame, Dk Ngawaru Maghembe, Alhaj Adam Kimbisa. Kwa upande wa upinzani chama cha CUF ni Habib Mnyaa.

Dar es Salaam. Bunge jana limewachagua wabunge sita kuiwakilisha Tanzania katika bunge la Afrika Mashariki (Eala)

Wabunge waliopita kwa kupigiwa kura kwa upande wa CCM  ambao ni kundi A ni  Fancy Nkuhi, Happines Legiko, Maryam Ussi Yahya, Dk Abdullah Makame, Dk Ngawaru Maghembe, Alhaj Adam Kimbisa. Kwa upande wa upinzani chama cha CUF ni Habib Mnyaa.

Hata hivyo, wanachama wawili walioteuliwa na Chadema kuwania ubunge wa Eala, Ezekiah Wenje alipata kura 124 za ndiyo na 174 za hapana na Laurence Manja, alipata kura 124 za ndiyo na 198 za hapana.