JKCI yafanya upasuaji valvu za moyo kwa wagonjwa 20

Timu ya madaktari waliofanya upasuaji .Picha na Herieth Makweta

Muktasari:

  • JKCI kwa mara kwanza imefanya  upasuaji huo kwa  wagonjwa 20.

Dar es Salaam. Jopo la madaktari wa upasuaji wa moyo katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) imefanya upasuaji wa kihistoria upasuaji wa kutanua valvu za moyo kwa kushirikiana na daktari bingwa wa upasuaji moyo kutoka India Subhash Chandra.

JKCI kwa mara kwanza imefanya  upasuaji huo kwa  wagonjwa 20.

"Tulianza jana na mpaka leo tumefanikiwa kufanya upasuaji kwa wagonjwa 16 na leo tutakamilisha kwa wagonjwa wote kwa kuwa jumla yao ni 20," amesema daktari bingwa Peter Kisenge.