VIDEO: Mambo 7 makuu kuhusu Boeing 737 Max-8

Muktasari:

  • Ni ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia iliyoanguka jana wakati ikianza safari kuelekea Nairobi

Mashirika. Boeing 737 Max-8 imekuwa katika safari za kibiashara tangu mwaka 2017.

Injini yake iko mbele kidogo na juu kiasi na usawa wa mbawa zake, ikilinganishwa na muundo wa awali wa ndege za Boeing.

Kifaa cha kubaini ajali na kazi ya programu inayoendesha kazi hiyo inafanya kazi tofauti na ile ya miundo ya awali ya Boeing 737.

Ndege iliyoanguka ni miongoni mwa sita kati ya 30 zilizoagizwa na Shirika la Ndege la Ethiopia kwa upanuzi wa shirika hilo.

Ajali nyingine ya ndege kama hiyo ya shirika la Lion Air ambayo pia ilikuwa mpya ilitokea muda mfupi baada ya kuondoka.

Boeing ilisema imetuma ilani ya dharura kwa kampuni za ndege ikionya kuhusu matatizo ya mfumo wa kuzuia ndege kukosa nguvu.

Katika ajali ya nyuma, marubani walionekana kutatizika na mfumo huo wa kujitegemea ulioundwa kuizuia ndege hiyo kukwama, ulioidhinishwa katika Boeing 737 Max.