Mfuriko yaua 154 nchini India

Sunday August 11 2019

 

India. Idadi ya vifo vilivyotokana na mafuriko mapya yaliyoambatana na dhoruba kali nchini India imefikia watu 154.

Inaelzwa kuwa mafuriko hayo pia yameathiri wakazi zaidi ya milioni moja baada ya makazi yao kuharibiwa vibaya.

Kwa mujibu wa Shirika la habari la BBC, Katika jimbo la Kerala lililopo Kusini mwa India watu 60 wamepotiza maisha kutokana na mafuriko hayo yaliyoanza siku ya Alhamisi.

Serikali nchini India imeshawahamisha wakazi 22, 900 katika kambi za muda.

Maafisa wa kupambana na maafa nchini humo walisema hali ya mafuriko bado ni mbaya huku vifo zaidi vikiripotiwa katika wilaya za Wayanad na Malappuram zilizokumbwa na maporomoko kutokana na mvua kubwa.

Vikosi vya uokoaji, jeshi la nchi kavu na la wanamaji pamoja na vikosi vya anga, vimepelekwa katika majimbo yaliyoathiriwa ili kuendelea na shughuli za uokoaji na kutoa misaada.

Advertisement

Msimu wa dhoruba kali nchini India huwa kati ya mwezi Juni na Septemba ambako mvua kubwa husababisha uharibifu na vifo.

Advertisement