Ndugu wa waliopoteza maisha kusaidia utambuzi Ethiopia

Muktasari:

  • Katika hatua nyingine, ndege zote za Ethiopia zinazohusisha Boeing 737 MAX 8 zimesitisha safari zake kwa sababu za kiusalama na uchunguzi kuhusu sababu za ajali ya Jumapili

Nairobi, Kenya. Waziri wa Usafirishaji, James Macharia wa Kenya amesema Serikali itawasafirisha kuelekea Ethiopia ndugu wa waliopoteza maisha kwa ajali ya ndege mjini Addis Ababa ili waweze kusaidia kutambua miili.

Akizungumza na waandishi wa habari, Macharia amesema familia 25 kati ya 32 tayari wamepatiwa taarifa na taratibu za kupata familia zilizobaki zinaendelea.

Waziri amesema, zoezi la usafirishaji litafanywa kwa ushirikiano na Serikali ya Ethiopia na Kenya pia mashirika ya ndege ya Kenya Airways na Ethiopian Airlines.

Ethiopian Airlines, walitangaza kusafirisha miili kuelekea Kenya baada ya kumaliza shughuli za uthibitisho.