Uwanja wa ndege wa Hong Kong wafunguliwa

Wednesday August 14 2019

 

Hong Kong, China. Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hong Kong umefunguliwa rasmi baada ya kufungwa na siku mbili za mapigano makali kati ya polisi na waandamanaji.

Mamlaka hiyo ilisema shughuli za uwanja huo zilirejea tena leo asubuhi baada ya mapigano kati ya waandamanaji wa na polisi walifunga kizuizi cha kusafiri kwa siku mbili kusitishwa.

Hata hivyo, mamlaka hiyo ambao ni mojawapo ya viwanja vikubwa kabisa duniani ilisema maandamano hayo yameathiri kwa kiasi kikubwa shughuli za uwanja huo.

Kwa mujibu wa Shirika la habari la BBC, mageti ya ukaguzi yalifunguliwa na kuruhusu mamia ya wasafiri waliokuwa wamekwama kwa siku mbili mfululizo kuanza safari zao.

Hata hivyo, Jarida la Asubuhi la China Kusini lilisema kuwa  waandamanaji wapatao 50 waliendelea kukaa katika uwanja huo ingawa hawakuwa na madhara yoyote kwa abiria.

“Tulipata amri ya muda ya kuwazuia watu waliokuwa wakizuia shughuli za uwanja kwa makusudi,” ilisema taarifa hiyo na kuongeza kuwa kwa sasa maandamano hayo yamepigwa marufuku katika eneo lolote la uwanja huo.

Advertisement

Kwa zaidi ya miezi mitatu sasa wananchi wa visiwa vya Hong Kong wanaandamana kudai demokrasia ikiwa ni pamoja na kupinga mswada ambao ungeruhusu watuhumiwa kushtakiwa kwa sheria za China bara.

Mapema jana usiku waandamanaji hao walikabiliana nyingine, na polisi baada ya kutaka kuzuia magari ya polisi kuingia uwanjani hapo.

Baadhi ya maafisa wa polisi walitumia ngao za kujikinga na risasi na kuwasukuma nyuma waandamanaji na kuwanyunyizia maji yenye pilipili kuwatawanya.

Advertisement