Wanajeshi Sudan waua mmoja

Muktasari:

Mauaji hayo yametokea siku ya Jumapili wakati kundi la wandamanaji waliokuwa wakipinga uwepo wa wanajeshi kwenye mji wa El-Souk.

Khartoum, Sudan. Jeshi nchini Sudan linadaiwa kumuua raia mmoja katika eneo la Kusini Mashariki mwa mji mkuu Khartoum.

Mauaji hayo yalitokea jana Jumapili Julai 15, wakati kundi la wandamanaji waliokuwa wakipinga uwepo wa wanajeshi kwenye mji wa El-Souk kudhibitiwa.

Watu walioshuhudia tukio hilo walisema mauaji hayo yalitokea wakati wakazi wa Jimbo la Sinnar walipoandamana kushinikiza vikosi vya RSF kuondoka kwenye mji huo.

Kwa mujibu wa Shirika la habari la AFP, awali wanajeshi hao wa RSF walipiga risasi za moto hewani lakini baadae waliwafyatulia raia na kusababisha kifo cha mtu mmoja na kujeruhi wengine kadhaa.

Shuhuda huyo alisema wakati wa maandamano hayo, wanajeshi walivamia ofisi za umoja wa vijana na kuwapiga.

Kufuatia mauaji hayo leo wananchi wa nchi hiyo wameandamana katika miji mbalimbali kuomboleza waliouawa kwenye shambulizi hilo.