Wapinzani Sudan wakataa uchaguzi

Muktasari:

  • Hatua hiyo inakuja siku moja baada ya jeshi la nchi hiyo kutangaza Uchaguzi Mkuu wa kupata rais mpya baada ya miezi tisa

Khartoum, Sudan. Viongozi wa waandamanaji nchini Sudan wameitisha maandamano mapya na kukataa mpango wa uchaguzi mpya uliotangazwa na baraza la kijeshi.

Jana Jeshi la Sudan lilitangaza kuvunja makubaliano yote baina yake na wapinzani na kuingia katika uchaguzi wa kupata rais mpya baada ya miezi tisa.

Kufanyika kwa uchaguzi huo kunafuatia aliyekuwa Rais wanchi hiyo Omar al-Bashir kung’olewa madarakani mwezi Aprl kufuatia maandamano yalytofanywa na wananchi kwa mwei mmoja wakishinikiza kuondoka kwake.

Makubaliano hayo yamekuja siku moja baada ya jeshi la nchi hiyo nkuwarushia risasi za moto waandamanaji waliokuwa mbele ya makao makuu jeshi hilo mjini Khartoum na kusababisha mauaji ya watu 35 na kujeruhi kadhaa.

Chama cha wanataaluma wa Sudan ambacho kiliratibu upinzani uliomuondoa madarakani Rais Omar al-Bashir kimesema siyo baraza la wanajeshi, wala wanamgambo washirika wake, watakaomua mustakabali wa watu wa Sudan, wala namna mchakato wa kuelekea kwenye utakavyoendeshwa.

Aidha, makundi ya waandamanaji yamezionya baadhi ya nchi za kiarabu dhidi ya kuingilia katika masuala ya ndani ya Sudan na kuzitaka kuacha kuunga mkono wanajeshi.

Onyo hilo linaaminika kuzilenga Saudi Arabia, Umoja wa Falme za Kiarabu na Misri, ambazo wachambuzi wanasema zinajaribu kuimarisha ushawishi wao nchini Sudan baada ya kuangushwa kwa utawala wa Rais Omar al-Bashir.