Takukuru yataja sababu za kumkamata Nyalandu

Dar es Salaam. Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru), imemkamata aliyewahi kuwa Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu na wenzake waweili ikiwatuhumu kwa rushwa na kufanya mikutano isiyoruhusiwa.
Awali, Mkurugenzi wa Mambo ya Nje, Itikadi na Uenezi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mrema alisema watu wawili waliojitambulisha kama askari Polisi walifika Kata ya Itaja Singida Kaskazinina kuwakamata wakidai kuwapeleka makao makuu ya Polisi Mkoa wa Singida.
Aliwataja makada wengine wa chama hicho waliokamatwa kuwa David Jumbe ambaye ni Mwenyekiti wa kata ya Itaja, na Mwenyekiti wa kijiji, Peter Mwangu.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida alipoulizwa kwa simu alikanusha jeshi hilo kuwakamata akiitaja Takukuru.

Akizungumza kwa simu na Mwananchi, Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Singida, Joshua Msuya alisema Nyalandu na wenzake wamekamatwa kutokana na tuhuma za rushwa na kufanya mikutano isiyoruhusiwa.

“Sisi tulikuwa tunafuatilia taarifa zinazohusiana na vitendo vinavyofanyika ambavyo vinaashiria matukio yasiyo ya kawaida kabla ya uchaguzi. Hicho tu,” alisema Msuya.

“Kwa mfano, kujihusisha na vitendo vya rushwa, kutoa hela, kufanya mikutano isiyoruhusiwa iya nyumba kwa nyumba. vitendo kama hivyo tunafuatilia,” aliongeza akisema wamepata malalamiko kutoka kwa wananchi.

Alisema baada ya kuwahoji wamewahamishia Polisi kwa hatua zaidi,