Aibuka na Sh15 milioni za promosheni miaka mitano ya MPAWA

Dar es Salaam. Benki ya CBA na Vodacom wamefunga promosheni ya kusherehekea maadhimisho ya miaka mitano ya MPAWA leo huku kukishuhudiwa mshindi aliyeibuka na zawadi ya Sh15 milioni.
Droo hiyo kubwa na ya mwisho iliendeshwa kwenye makao makuu ya benki ya CBA yaliyopo Posta jijini
Dar es salaam mbele ya ofisa kutoka Bodi ya Michezo ya Bahati Nasibu, Humudi Hussein, wawakilishi kutoka, CBA, Yessie Yassin na Maria Marbella, mwakilishi kutoka Kampuni ya
Vodacom, Alice Lushiku.
Andrisa Mathias kutoka Geita ndiye aliibuka mshindi mkubwa wa promosheni hii kubwa ya akiondoka na Sh15 milioni.
Akiongea na waandishi wa habari, mwakilishi mkuu wa MPAWA benki  ya CBA, Gloria Njiu
alisema “MPAWA ni huduma inayolenga kuwaendelea na kuwawezesha watanzania wengi hususani
wasiofikiwa na huduma za kibenki pamoja na wajasiriamali wadogo na maadhimisho haya ya miaka mitano
yanalenga kuwawezesha na kuwashukuru wapendwa wateja wetu wote.”
Aliongezea kuwa Benki ya CBA
inajivunia safari hiyo ya miaka mitano ya mafanikio ya huduma hii na kuwapongeza wateja wote walioshinda
hususani Andrisa ambaye ni mshindi mkubwa wa promosheni hii.
Akiongea kwa njia ya simu, mshindi huyo wa alionyesha furaha za waziwazi na kutoa shukrani zake kwa benki ya CBA na kampuni ya Vodacom kwa kuanzisha huduma hiyo.
Mwakilishi kutoka Vodacom, Alice Lushiku pia alitoa neno lake akisema “Tunawapongeza washindi wote na tunaendelea kuwahimiza waendelee kuhifadhi akiba zao, kurudisha mikopo yao mapema na kwa watu wote ambao sio wateja wa MPAWA tunawahimiza kujiunga na huduma hii
inayowasadia kuwajumuisha katika ulimwengu wa kifedha hususani kwa watu ambao hawafikiwi na huduma za kibenki kwa urahisi.”