Akamatwa na vipande 213 ya nyama ya nyumbu

Muktasari:

  • Mtumishi wa hifadhi ya wanyamapori ya Ikona mkoani Mara amekamatwa na vipande 213 vya nyama ya nyumbu kambini.

Serengeti. Mtumishi wa hifadhi ya wanyamapori ya Ikona iliyoko wilaya ya Serengeti mkoani Mara, Thomas Mugabo (56) amekamatwa na vipande 213 vya nyama ya nyumbu kambini kwao.

Meneja wa mapori ya Akiba ya Ikorongo na Grumeti, Nollasco Ngowe akizungumza na Mwananchi jana Jumatatu Juni 24,2019 alisema mtumishi huyo alikamatwa jana saa 2 usiku.

Ngowe alisema mtumishi huyo watamkabidhi kwa polisi kwa hatua zaidi dhidi.

Mmoja wa askari jina aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema nyara hizo zilikutwa kambini hali inayoonyesha askari na watumishi wenye dhamana ya ulinzi ndiyo wanahusika na vitendo hivyo.