Alichokisema Dk Kigwangalla kuhusu sanamu ya Nyerere

Wednesday July 10 2019

 Dk Kigwangalla , sanamu  Nyerere, Hifadhi ya Taifa , Burigi-Chato mkoani Geita,

 

By Tumaini Msowoya, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Bila shaka utakuwa umeiona sanamu ya Julius Nyerere iliyowekwa katika lango kuu la kuingia Hifadhi ya Taifa ya Burigi-Chato mkoani Geita.

Baada ya uzinduzi wa hifadhi hiyo jana Jumanne Julai 9, 2019 uliofanywa na Rais John Magufuli, mjadala uliibuka katika mitandao mbalimbali ya kijamii kuwa sanamu haifanani na mwonekano wa Rais wa Awamu ya Kwanza.

Lakini Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla kupitia video inayosambaa mitandaoni amesema kama kuna upungufu wizara hiyo kwa kushirikiana na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ndiyo wenye dhamana ya kuangalia kama ina kasoro ili ifanyiwe marekebisho.

Waziri huyo amesema wana wataalam watakaoitazama sanamu hiyo na kujua kama ina upungufu na kurekebishwa.

Miongoni mwa watu waliohoji suala hilo ni  

Malisa GJ ambaye katika ukurasa wake wa facebook ameandika ”Tatizo sio mchonga kinyago,  tatizo ni mtoa maelekezo, mchongaji aliambiwa chonga kinyago cha Nyerere,  hakuambiwa Nyerere yupi.”

Advertisement

 


Advertisement