Bunge la Uingereza limekataa kujiondoa Brexit

Spika John Bercow

Muktasari:

London,Uingereza. Wabunge wa Uingereza wamekataa makubaliano ya Waziri Mkuu Theresa May na Umoja wa Ulaya kuhusu Uingereza kujiondoa kutoka kwenye Umoja huo, jambo lililouvuruga mchakato wa Brexit.


Kushindwa kwa Waziri Mkuu Theresa May  kulitarajiwa na wengi ingawa kiasi cha kura alizoshindwa nazo ni jambo ambalo limeuharibu uongozi wake

London,Uingereza. Wabunge wa Uingereza wamekataa makubaliano ya Waziri Mkuu Theresa May na Umoja wa Ulaya kuhusu Uingereza kujiondoa kutoka kwenye Umoja huo, jambo lililouvuruga mchakato wa Brexit.

Hatua hiyo ilisababisha  kura isiyokuwa na imani kuwasilishwa, hatua ambayo inaweza kuiangusha Serikali ya May. Wabunge walioyapinga makubaliano hayo ni 432 huku walioyaunga mkono wakiwa 202 pekee.

Kushindwa kwa Waziri Mkuu huyo kulitarajiwa na wengi ingawa kiasi cha kura alizoshindwa nazo ni jambo ambalo limeuharibu uongozi wake.

Kushindwa huku ni kwa kihistoria kwa kuwa ndiyo mara ya kwanza kwa Serikali kushindwa kwa kiasi kikubwa cha kura katika bunge la nchi hiyo na kunafuatia msukosuko wa kisiasa wa zaidi ya miaka miwili ambapo May alijiwekea hadhi ya kisiasa kwa kuhakikisha amepata makubaliano ya Brexit.

Muda mfupi baada ya matokeo kutangazwa na Spika John Bercow Waziri Mkuu May, alizungumza.

"Ahsante  Spika.  Spika bunge limeshasema na Serikali itasikiliza. Ni wazi kwamba bunge haliungi mkono makubaliano haya ila kura ya usiku wa leo(jana) haituambii bunge linaunga mkono hasa kitu gani, haituambii chochote kuhusu ni vipi au hata ikiwa linaunga mkono uamuzi wa Waingereza katika kura ya maoni iliyoamuliwa na bunge hili. Na watu hasa raia wa Umoja wa Ulaya ambao wamefanya makao yao hapa na raia wa Uingereza wanaoishi katika nchi za Umoja wa Ulaya, wanastahili kupata uwazi kuhusiana na maswali haya haraka iwezekenavyo," alisema May.