CAG abaini wakulima kuuziwa viuatilifu badala ya kupewa bure

Muktasari:

  • CAG amebaini kuwapo kwa mapungufu mbalimbali katika pembejeo zenye thamani za Sh 19.9 bilioni zilizotolewa kwa wakulima wa pamba katika kipindi cha mwaka wa fedha 2017/18.

Dar es Salaam. Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) imebaini kuwapo kwa upungufu mbalimbali katika pembejeo zenye thamani za Sh19.9 bilioni zilizotolewa kwa wakulima wa pamba katika kipindi cha mwaka wa fedha 2017/18.

Ripoti ya CAG iliyowasilishwa bungeni Aprili 10, 2019 imebainisha upungufu huo ni pamoja na baadhi ya wakulima kupewa viuatilifu zaidi kuliko ukubwa wa mashamba yao.

"Sikuweza kuona nyaraka za kupokelea viuatilifu hivyo," imeonyesha sehemu ya ripoti hiyo.”

Mbali na upungufu huo CAG amebaini licha ya  Serikali kutoa ruzuku za pembejeo kwa ajili ya maendeleo ya kilimo kwenye baadhi ya maeneo aliyokagua, viuatilifu viliuzwa kwa wakulima badala ya kugawiwa bure kama ilivyoelekezwa na Bodi ya Pamba.

 "Sikuweza kuona uthibitisho wa saini za wakulima kupokea viuatilifu hivyo katika wilaya nilizofanya ukaguzi," amebainisha CAG.