Daktari azungumzia afya ya Mwigulu

Muktasari:

Jana Jumatano Februari 13, 2019 mbunge wa Iramba Magharibi (CCM), Mwigulu Nchemba alipata ajali na leo mkurugenzi wa hospitali ya Benjamin Mkapa alikolazwa mbunge huyo, amezungumzia afya yake

 


Dodoma. Afya ya mbunge wa Iramba Magharibi (CCM), Mwigulu Nchemba  anayetibiwa katika Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma baada ya kupata ajali ya gari jana Jumatano Februari 14, 2019 inazidi kuimarika.

Akizungumza leo Alhamisi Februari 14, 2019 mkurugenzi wa hospitali hiyo, Dk Alphonce Chandika amesema mbunge huyo anaendelea vizuri isipokuwa ana maumivu ya mgongo.

Waziri huyo wa zamani wa Mambo ya Ndani alipata ajali eneo la Migori mkoani Iringa wakati akielekea Singida katika mkutano wa kamati ya siasa ya Mkoa huo.

Chanzo cha ajali hiyo ni gari alilokuwa amepanda kugonga punda walikokuwa wakikatisha barabarani.