Kitwanga anasema ataendelea kupiga kelele hadi kieleweke

Wednesday August 14 2019

Mbunge wa Misungwi Charles Kitwanga,mwenye

Mbunge wa Misungwi Charles Kitwanga,mwenye shati la drafti akiteta jambo na mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira (Mwauwasa) mhandisi Antony Sanga. Kulia ni katibu mkuu wa wizara ya maji Profeaa Kitila Mkumbo. Picha na Jonathan Musa 

By Jonathan Musa, Mwananchi [email protected]

Misungwi. Mbunge wa Misungwi (CCM) nchini Tanzania, Charles Kitwanga amesema hawezi kuacha kupiga kelele wakati wananchi wake wanakabiliwa na shida.

Kitwanga ameyasema hayo leo Jumatano Agosti 14,2019 wakati akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Profesa Kitila Mkumbo kutembelea mradi wa maji wa Mapilinga uliopo Misungwi, unaotekelezwa na wizara kupitia Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (Mwauwasa).

Hii ni kufuatia ongezeko la ankara ya maji kutoka Sh14 ya awali hadi Sh24.50 kwMbunge wa Misungwi (CCM) nchini Tanzania, Charles Kitwanga amesema hawezi kuacha kupiga kelele wakati wananchi wake wanakabiliwa na shida.a ndoo moja yenye ujazo wa lita 20.

"Mimi nawawakilisha wananchi wangu, kama hawapati huduma inayostahili na uwezo upo ni lazima nitapiga kelele tu. Pia ni bora tuwe tunaambiwa," amesema Kitwanga aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya ndani

Aidha ameziomba mamlaka nyingine kujenga utaratibu wa kuuandaa wananchi kisaikolojia kabla ya kufanya mageuzi hususan yanayohitaji gharama au fedha.

Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa Mwauwasa, Antony Sanga amesema kabla ya bei hizo kupandishwa kwa matumizi ya nyumbani walilazimika kulipia Sh700 kwa unit moja na baada ya kupandishwa watalazimika kulipia Sh1, 225 kwa unit.

Advertisement

“Wanaopandisha bei za maji wengi wao ni wale wenye vituo vya kuuza maji na hawa ndio wanaeneza uongo ila ukweli ni kwamba bei ya maji haijapanda kiasi cha kumtisha mtu ashindwe kuchota maji,” amesema Sanga

Advertisement