Lukuvi awatangazia vita wadaiwa sugu kodi ya ardhi
Muktasari:
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amekutana na wakuu wa taasisi, mashirika na kampuni yanayodaiwa kodi ya pango la ardhi na kutoa siku tisa kwa wadaiwa sugu kulipa kodi hiyo, watakaoshindwa watafikishwa mahakamani
Dodoma. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi nchini Tanzania, William Lukuvi amesema wadaiwa sugu wa kodi ya ardhi wataanza kufikishwa mahakamani Juni 21, 2019.
Akizungumza leo Jumanne Juni 11, 2019 Lukuvi amesema kuna taasisi, kampuni na mashirika 207 yanadaiwa zaidi ya Sh200 bilioni.
“Wanatakiwa kulipa kabla ya Juni 20, 2019 ili kukwepa aibu na fedheha,”amesema Lukuvi.
Amesema kuanzia Juni 21, 2019 wasiolipa watafikishwa mahakamani kupitia madalali waliowateua kukamata, kuuza mali zao.
Lukuvi amesema wawakilishi kutoka taasisi 197 kati ya 207 aliowaita katika mkutano huo uliofanyika jijini Dodoma wamehudhuria.
Awali Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Makazi, Dorith Mwanyika amesema baada ya kuziita taasisi za Serikali walibaini ambazo hazijalipa kodi tangu mwaka 2012 hadi sasa