Magufuli awaapisha majaji

Rais wa Tanzania, John Magufuli 

Muktasari:

Rais wa Tanzania, John Magufuli leo Jumanne Januari 29, 2019 Ikulu jijini Dar es Salaam amewaapisha majaji sita wa Mahakama ya Rufani na majaji 15 wa Mahakama Kuu

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, John Magufuli leo Jumanne Januari 29, 2019 Ikulu jijini Dar es Salaam amewaapisha majaji sita wa Mahakama ya Rufani na majaji 15 wa Mahakama Kuu.

Katika uteuzi uliofanyika Januari 27, 2019 na taarifa yake kusomwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi, kiongozi mkuu huyo wa nchi alitengua uteuzi wa wakuu wa wilaya wawili  na kuteua wakurugenzi 10 ili kuziba nafasi zilizoachwa wazi kwenye halmashauri za mikoa mbalimbali nchini.

Majaji walioapishwa leo ni Cyprian Mkeha, Dunstan Ndunguru, Seif Kulita, Dk Mtemi Kilikamajenga,  Zeferine Galeba, Dk Juliana Masabo, Mustafa Ismail, Upendo Madeha, Wilbard Mashauri, Yohanne Masara, Dk Lilian Mongella, Fahamu Mtulya, John Kahyoza, Athumani Kirati na Suzan Mkapa wote wa Mahakama Kuu.

Majaji wa mahakama ya Rufani ni Sahel Barke, Dk Rehema Sameji, Dk Mary Levira, Ignas Kitusi, Winnie Korosso na Lugano Mwandambo.

Katika uteuzi wake huo Magufuli pia amemteua aliyekuwa kiongozi wa mbio Mwenge mwaka 2018, Charles Kabeho kuwa mkuu wa Wilaya ya Tarime kuchukua nafasi ya Glorias Luoga ambaye uteuzi wake umetenguliwa huku nafasi ya Aaron Mbogho aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Mwanga ikichukuliwa na Thomas Apson.

Wakurugenzi 10 wapya walioteuliwa ni Isaya Mbenje (Pangani), Dk Fatuma Mganga (Bahi), Regina Bieda (Tunduma), Jonas Malosa (Ulanga), Ali Juma Ali (Njombe), Misana Kangura (Nkasi), Diocres Rutema (Kibondo), Neto Ndilito (Mufindi), Elizabeth Gumbo (Itilima), Stephen Ndaki (Kishapu).