VIDEO: Magufuli azindua ofisi ya Rais Dodoma

Muktasari:

Baada ya kuwapo wazo la muda mrefu la Serikali kuhamishia shughuli zake Dodoma, hatimaye lengo limeanza kutimia na leo ofisi ya Rais imefunguliwa jijini humo

Dar es Salaam. Rais John Magufuli leo Jumamosi Aprili 13,2019 amezindua jengo la ofisi ya Rais lililopo eneo la Ikulu ya Chamwino Dodoma ikiwa ni mwendelezo wa utekelezaji wa agizo la Serikali kuhamia jijini humo.

Uzinduzi huo umeshuhudiwa na viongozi wakuu wa Serikali akiwamo Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  na Katibu mkuu kiongozi Dk John Kijazi.

Akitoa taarifa fupi ya ujenzi huo, Katibu wa Ikulu, Dk Moses Mpogole ameeleza kuwa jengo kuu katika ofisi hizo limejengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) huku majengo mengine 12  yakijengwa na Suma JKT.

Amesema ujenzi huo umefanyika ndani ya miezi 11 ukihusisha jengo kuu la ghorofa mbili lenye ofisi ya Rais, makamu wa Rais, katibu mkuu kiongozi pamoja na wasaidizi wengine wa Rais.