Majaliwa: Serikali haitawavumilia watumishi wa ovyo

Muktasari:

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema Serikali haitawaonea haya watumishi watakaoshindwa kutekeleza majukumu yao ya kuwatumikia wananchi na kuifanya ionekane ya ovyo

Moshi. Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema Serikali haitawaonea haya watumishi watakaoshindwa kutekeleza majukumu yao ya kuwatumikia wananchi na kuifanya ionekane ya ovyo.

Ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Julai 18, 2019 wakati akizungumza na watumishi wa Wilaya ya Moshi pamoja na sekretarieti ya Mkoa wa Kilimanjaro.

Amesema msimamo  wa Serikali ni kutowalinda watumishi wazembe, wezi, wavivu, wala rushwa na wabadhirifu.

"Sipendi kuona haya niliyoyataja hapa yanajitokeza, kazi ya mtumishi yeyote ni kutumikia wananchi na kuwapa majibu ya maswali na matatizo yao, mwasikilize wananchi wana shida gani na mwasaidie.”

"Msiwe sehemu ya kuifanya Serikali kuwa ya ovyo kwa kushindwa kutekeleza majukumu yenu na endapo itatokea hivyo hatutavumiliana. Ni matarajio yetu kuona mkiwasaidia na kuwasikiliza wananchi, "amesema Majaliwa.

Amebainisha kuwa kuona ubaguzi wa aina yoyote wa rangi, kabila au chama katika kutoa huduma kwa wananchi.