Majaliwa awabana mawaziri, ataka wahudhurie vikao vya kamati

Muktasari:

  • Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewapiga pini mawaziri na kuwataka kufika mbele ya kamati wakiitwa bila visingizio

Dodoma. Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewaagiza mawaziri wote kuwepo Dodoma wakati wa vikao vya kamati bila visingizio.

Majaliwa ametoa kauli hiyo leo Jumanne Machi 12, 2019 Jijini Dodoma wakati akifungua kikao cha Bunge kwa ajili ya kujadili ukomo wa bajeti ya Serikali ya mwaka 2019/2020.

Amewaambia wenyeviti wa kamati kuwa, wakati wowote wakiwahitaji mawaziri wawaite kwani Serikali ilishatoa maelekezo lazima wafike mbele ya kamati wakiitwa.

"Sisi serikalini tulishatoa maelekezo kuwa kila waziri akihitajika mbele ya kamati lazima afike bila kisingizio, hivyo mkiwahitaji waiteni wapo," amesema Majaliwa.

Majaliwa pia amewataka wabunge kuhudhuria kwa wingi vikao vya kamati na kutumia muda huo kujadili shughuli za maendeleo.