VIDEO: Mfanyabiashara Akram Azizi kizimbani, asomewa mashtaka 75

Mfanyabiashara Akram Azizi  akitoka katika chumba cha hakim mkazi kisutu kusomewa mashtaka 75 utakatishaji fedha kukutwa nyara za serikali na kukutwa na silaha

Muktasari:

Mfanyabiashara Akram Azizi  amefikishwa  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka 75 ya uhujumu uchumi, ikiwamo kukutwa na nyara za Serikali, silaha, risasi na utakatishaji wa fedha Dola za Marekani 9,018.

Dar es Salaam. Mfanyabiashara Akram Azizi amefikishwa  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka 75 ya uhujumu uchumi, ikiwamo kukutwa na nyara za Serikali, silaha, risasi na utakatishaji wa fedha Dola za Marekani 9,018.

Mshtakiwa anakabiliwa na mashtaka 70 ya kukutwa na silaha, mawili ya kukutwa na risasi, mawili ya kukutwa na nyaraka na moja la utakatishaji wa fedha.

Mshtakiwa huyo amesomewa mashtaka hayo na mawakili wa Serikali wakuu,  Paul Kadushi na Faraja Nchimbi mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi,  Augustine Rwizile.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo mshtakiwa huyo hakuruhusiwa kuongea chochote kwa sababu mahakama hiyo ya Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo hadi Mahakama Kuu.

Hata hivyo kwa mujibu wa sheria shtaka la utakatishaji  fedha halina dhamana.

Upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika, kesi hiyo imeahirishwa hadi  Novemba 12, 2018.