Mtoto wa Zidane apelekwa Santander kwa mkopo

Wednesday July 10 2019

Mtoto  Zidane, apelekwa Santander ,mkopo,Real Madrid, Luca Zidane ,

Luca Zidane 

Madrid, Hispania (AFP). Real Madrid imetangaza kuwa mtoto wa kocha wao mkuu, Luca Zidane amejiunga na timu ya daraja la pili ya Racing Santander kwa mkopo kwa msimu ujao.

Luca Zidane, kipa mwenye umri wa miaka 21, ni matunda ya mfumo wa vijana wa klabu hiyo, pamojana kaka yake Enzo, na wote wameshafundishwa na baba yao, Zinedine.

Muda mfupi baada ya kurejea Real kuwa kocha mwezi Machi, Zidane alimpa nafasi Luca kwenye kikosi cha kwanza katika mechi dhidi ya Huesca iliyofanyika Uwanja wa Santiago Bernabeu na Real kushinda kwa mabao 3-2, hiyo ikiwa ni mara ya pili kupangwa kikosi kinachoanza.

Luca Zidane alitwaa ubingwa wa Mataifa ya Ulaya ya wachezaji wenye umri chini ya miaka 17 akiwa na Ufaransa mwaka 2015.

 


Advertisement

Advertisement