Nape Nnauye ajiuzulu uenyekiti wa kamati ya Bunge

Muktasari:

Ofisi ya Spika wa Bunge la Tanzania imethibitisha kupokea barua ya mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye ya kujiuzulu nafasi ya Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Nape Nnauye leo Jumatatu Februari 04,2019 ameandika barua kwenda kwa Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai ya kujiuzulu nafasi hiyo.

Akizungumza na Mwananchi kwa simu leo Jumatatu saa 2 usiku, Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai amethibitisha kuiona barua ya Nape ambaye ni mbunge wa Mtama (CCM) ya kujizulu nafasi hiyo.

“Ni kweli na mimi barua nimeiona,” amesema  Kagaigai

 

Endelea kufuatilia Mwananchi kujua undani wa habari hii