Nay wa Mitego amwaga noti kwa kina mama Manzese

Thursday November 29 2018

 

By Nasra Abdallah

Msanii Elibariki Emmanuel maarufu Ney wa Mitego, amewatembelea wajasiriamali wanawake  zaidi ya 70 wanaofanya shughuli zao katika eneo la Manzese, jijini Dar es Salaam  kwaajili ya kuzungumza na kusikiliza kero zao.

Ney wa Mitego alianza shughuli hiyo leo Novemba 29 majira ya 3:00 asubuhi akiwa ameongozana na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa  Midizini, Mohamed Mkumba na Mwenyekiti wa mtaa wa Muungano, Joseph Mkude .

Amesema ameamua kufanya hivyo ili kukumbuka alipotoka, kwani yeye pamoja na ndugu zao walilelewa na mama yao peke yake baada ya baba kufariki huku akiwa anafanya kazi za mama lishe.

Alieleza kuwa hata wimbo wake wa hivi karibuni 'Hakuna Maisha Magumu' ulikuwa ni wazo la mama yake.

Mbali na Manzese, Ney wa Mitego amesema ana mpango wa kukutana na kina mama wote wa Wilaya tano za Mkoa wa Dar es Salaam.

Merina Sameje anayefanya biashara ya kuuza chapati, alimshukuru msanii hiyo na kueleza kuwa mtaji wa Sh50,000 aliompatia utamuwezesha kununua ndoo ya mafuta na mfuko wa unga wa ngano.

Merina amesema swali alikiwa hana uwezo huo kwani ulikuwa akipata bidhaa hizo kwa mali kauli.

Naye Husna Maulid anayejishughulisha na kupika supu, amesema wamekuwa wakidhilumiwa na wateha mara kwa mara jambo linalchangia kuua mtaji wao.

Husna alimuombea Mungu Nay aongezewe pale palipopungukiwa na kuongeza kuwa kuwakumbuka kina mama ni kuikumbuka famolia nzima.

Mitaa ambayo Ney ametembelea ni  Muungano, Midizini, Kilimahewa na Sisi Kwa Sisi.

 Advertisement