Ndege ATCL zaanza kukodishwa kibiashara

Muktasari:

  • Katika mitandao ya kijamii ziliibu-ka hisia tofauti pengine hali hiyo ni kutokana na ATCL kutozindua safari zake kwenda Nairobi.Hata hivyo, mkurugenzi wa ATCL, Ladislaus Matindi jana alisema shirika hilo linafanya biashara ya usafiri wa ndege hivyo si ajabu kuio-na popote. “Popote unapoona ndege yetu ina abiria au mizigo ujue tuna-fanya biashara,” alisema.

Dar es Salaam. Ndege aina ya Airbus A220-300 ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) imekodiwa kupeleka watu Nairobi nchini Kenya kisha kuwarudisha na kuendelea na ratiba nyingine kama kawaida.

Juzi ndege hiyo yenye nakshi za rangi ya bluu na nyeupe, mchoro wa twiga kwa nyuma na maandishi yas-omekayo Air Tanzania The Wings of Kilimanjaro ilionekana katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta nchini Kenya.

Flight radar (programu ya kufua-tilia urukaji wa ndege) inaonyesha ndege hiyo iliruka katika Uwanja wa Jomo Kenyatta saa 12:00 jioni kabla ya kurudi nchini.Ukodishaji wa ndege kwa ajili ya kubeba watu au mizigo ni utara-tibu wa kawaida katika mashirika mbalimbali ulimwenguni na huin-giza fedha nyingi.

Katika mitandao ya kijamii ziliibu-ka hisia tofauti pengine hali hiyo ni kutokana na ATCL kutozindua safari zake kwenda Nairobi.Hata hivyo, mkurugenzi wa ATCL, Ladislaus Matindi jana alisema shirika hilo linafanya biashara ya usafiri wa ndege hivyo si ajabu kuio-na popote. “Popote unapoona ndege yetu ina abiria au mizigo ujue tuna-fanya biashara,” alisema.

Hata hivyo chanzo cha kuaminika kililieleza gazeti hili kuwa, ndege hiyo ilikodiwa na watu wa Airbus bila kubainisha kama ilichukuliwa kwa ajili ya maonyesho ya ndege (Airshow) jijini Nairobi au matumizi mengine.

Tanzania inamiliki Airbus A220-300 mbili na ni nchi ya kwanza barani Afrika kuwa na ndege hizo.