VIDEO: Nyanzala anayeigiza sauti ya mke mdogo wa Sultan

Ni tamthilia inayohusu maisha ya Sultan Suleyman. Katika umri wa miaka 26 alianza mbio za kuitengeneza himaya yake ya Ottomans akitaka iwe kubwa kuliko ya Alexander the Great. Utawala wake wa miaka 46 ulihitajika ulimwenguni kote akiwa na Pargali Ibrahim….

Kuhusu Mahidevran Sultan

Katika tamthilia hii anaigiza kama nyumba ndogo ya Sultan Suleyman na mama wa Şehzade Mustafa.

Jina halisi la Mahidevran ni Asiye Nur Fettahoğlu. Ni mwigizaji, mwanamitindo na mtangazaji wa televisheni mwenye asili ya Uturuki na Ujerumani.

Nyanzala Kilima

Katika tamthilia hii, Nyanzala anaigiza kwa Kiswahili sauti ya Mahidevran Sultan, ambaye ni mmoja wa wake wa Sultan na mama wa Sehzade Mustafa.

“Huwa nafikiria yale maisha katika hali halisi, kwamba Mahidervan ndio mimi, najikuta namtukana tu Sultan, na najikuta napata wakati mgumu katika kupigana na hisia mpaka pale napojisemesha kuwa natakiwa nijue ule ni mchezo,” anasema Nyanzala mwenye umri wa miaka 23.

Changamoto anayokutana nayo ni kuwa kuna wakati anakuwa katika hali tofauti (mood) na hivyo kujikuta anashindwa kutimiza wajibu wake ipasavyo.

Mbali na kazi hiyo anasema huwa anajishughulisha na ujasiriamali na uigizaji na filamu aliyocheza ni ‘Mpango Mbaya”.

Hata hivyo anaeleza katika sanaa, kwa sasa anatazamia zaidi kuwa mtayarishaji kuliko kuwa mwigizaji.