RC Mara amwambia dereva wake aache kuwazia gari, bali kifo cha mtoto wake

Mkuu wa mkoa wa Mara, Adam Malima

Muktasari:

  • Mkuu wa mkoa wa Mara, Adam Malima amemtaka dereva wake kutofikiria thamani ya gari lililopata ajali, bali kifo cha mtoto wake aliyekuwa akiliendesha

Musoma. Mkuu wa mkoa wa Mara, Adam Malima amemtaka dereva wake kutofikiria thamani ya gari lililopata ajali, bali kifo cha mtoto wake aliyekuwa akiliendesha.

Pia, Malima alimwambia dereva huyo, Shida Masaba, kuwa yuko tayari hata kutumia pikipiki ya magurudumu matatu, maarufu kwa jina la Bajaj, wakati Serikali ikimtafutia gari jingine.

Mtoto wa dereva huyo, Kasobi Shida alifariki akiwa hospitalini baada ya kuumia kwenye ajali iliyotokea Agosti 4, 2019  eneo la Kigere wakati akiendesha gari hilo la Serikali.

Akizungumza katika Ibada ya mazishi ya mtoto huyo jana, Malima alisema uhai Kasobi una thamani kubwa zaidi kuliko thamani ya gari hilo la Serikali.

Alisema tangu ateuliwe kuwa mkuu wa mkoa miaka miwili iliyopita, amekuwa akiendeshwa na Masaba kwa kutumia gari hilo wakitimiza kilomita 80,000 ambazo zilikuwa na misukosuko ya ajali na mikasa tofauti.

“Shida narudia tena kukwambia, usiwazie kuhusu gari,” alisema Malima.

 

Kwa habari zaidi soma gazeti la Mwananchi la leo Alhamisi Agosti 8, 2019