Rubani wa Makamu wa Rais Kenya afariki

Monday March 4 2019

 

Turkana,Kenya. Rubani wa Makamu Rais wa Kenya Williamu Ruto amekufa kwenye ajali ya helikopta  akiwa na abiria wane raia wa Marekani mara baada ya ndege hiyo kuanguka eneo la Lobolo.

Kwa mujibu wa polisi Rubani huyo aliyefahamika kwa jina la Mario Magonga  akiwa na abiria wake hao walipata ajali hiyo leo saa  mbili asubuhi.

‘’Polisi waliichukua miili ya watu watano ambayo ilipatikana eneo hilo ambapo mmoja wapo ni raia wa Kenya rubani wa makamu wa Rais Mario Magonga’’alisema taarifa ya polisi

 Taarifa hiyo ilisema  mpaka sasa chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika lakini mpaka baadaye uchunguzi unaofanywa na polisi utabainika nini hasa chanzo cha ajali hiyo.

Advertisement