Tanapa yaja na njia nyingine utalii wa kupanda Mlima Kilimanjaro

Mshauri wa masuala ya uhifadhi kutoka Shirika la hifadhi za Taifa nchini Tanzania, Ibrahim Mussa akitoa mada katika wa wahariri na waandishi waandamizi Kijiji Mwanza

Muktasari:

Mamlaka inakusudia kuanzisha utalii huo wa kupanda Mlima Kilimanjaro kwa kutumia njia hiyo ya Cable.

Mwanza. Mshauri wa Utalii toka Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (Tanapa), Ibrahim Mussa amesema kutumika kwa utalii wa Cable hakutaondoa uhalisia wa utalii kwa watalii watakao enda kupanda Mlima  Kilimanjaro kwa njia iliyozoeleka.

Hayo ameyasema leo Ijumaa Julai 5, 2019 mkoani Mwanza, Tanzania kwenye mkutano baina ya Tanapa na Wahariri na waandishi waandamizi wa vyombo mbalimbali vya habari nchini.

Mussa amesema mamlaka hiyo inakusudia kuanzisha utalii huo wa kupanda Mlima Kilimanjaro kwa kutumia njia hiyo ya Cable.

Mkutano huo ulianza Jana Alhamisi Julai 4, 2019 na ulifunguliwa na Waziri wa Maliasili na Utalii,  Dk Hamis Kingwangala.