Tanzania kuwasilisha ripoti UN

Wednesday March 20 2019

 

By George Njogopa, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Tanzania itawasilisha kwa mara ya kwanza ripoti ya tathmini kuhusu utekelezaji wa malengo endelevu ya maendeleo (SDG) kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mwaka huu.

Hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa makubaliano ya Umoja wa Mataifa yanayotaka kila nchi mwanachama kuweka mkakati ambao unaainisha namna inavyotekeleza malengo hayo yatayofikia ukomo 2030.

Kwa mujibu wa mwakilishi mkazi wa UN nchini, Alvaro Rodriguez, hakuna nchi inaweza kujihesabu iko salama kama itafikiria utekelezaji wa malengo hayo ni jukumu Umoja wa Mataifa pekee.

“Hii itakuwa ni mara ya kwanza Tanzania inawasilisha ripoti yake kueleza kile ilichokifanya hadi sasa na changamoto inazokabiliana nazo katika kutekeleza malengo hayo,” alisema wakati akizungumza na wawakilishi kutoka mashirika ya kijamii.

Naye mkurugenzi msaidizi kutoka Wizara ya Fedha, Servus Sagday alisema Serikali inaendelea kupokea ushauri utakaofanikisha uwasilishaji ripoti hiyo UN.

Advertisement