Tuzo ya utalii kutua Serengeti

Muktasari:

Wakazi wa Wilaya ya Serengeti kupokea tuzo ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kama ishara ya kuonyesha heshima

Serengeti.  Tuzo iliyotolewa na taasisi ya  World Travel ya nchini Mauritius kwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti baada ya kuwa bora Afrika, itapokelewa kesho na wakazi wa Wilaya ya Serengeti.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumatatu Juni 18, 2019 kwa njia ya simu Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Nurdin Babu amesema itapokelewa katika kijiji cha Robanda na itahusisha wadau mbalimbali kutoka mikoa ya Mara na Simiyu.

“Waziri wa Maliasili na Utalii Dk Khamisi Kigwangala ndiye atakuwa mgeni rasmi,ni heshima kubwa kuletwa huku maana hapa ndipo makao makuu ya Hifadhi, baada ya hapo itapelekwa kwa Rais Dk John Magufuli,” amesema.

Amesema tuzo hiyo inawapa wajibu mkubwa kama wilaya kuzidisha ulinzi kwa ujangili na wanaongiza mifugo usiku, kufanya hivyo kutaifanya kuendelea kuwa bora duniani.

Menasi Kiruri mmoja wa wafanyabiashara wa Mugumu amesema kwao ni heshima kubwa na kuomba tuzo hiyo itumike kuimarisha mahusiano ya wa Hifadhi na jamii inayowazunguka.