Vuguvugu la Uchaguzi Mkuu Kenya laibua mtikisiko wa Katiba

Ukifuatilia mambo yanavyokwenda kasi katika siasa za Kenya, hasa ukiwa hapa nchini, huwezi kuamini kwamba nchi hiyo itaingia katika Uchaguzi Mkuu unaofuata mwaka 2022, ikiwa ni miaka miwili baada ya Tanzania kufanya uchaguzi wake Oktoba 2020.

Kwa jinsi hali ilivyo, hapa mitaani vijana wanasema “mambo ni mengi muda ni mchache”. Kila siku linaibuka jipya na ukifuatilia kiini cha yote hayo ni Uchaguzi Mkuu.

Kama tulivyowahi kuandika hapa, yapo masuala ya mgawanyiko wa wazi kati ya Rais Uhuru Kenyatta na Naibu wake, William Ruto; ushirika unaoshangaza wengi kati ya Rais na Kiongozi wa upinzani, Raila Odinga; tofauti na Raila na Ruto; makundi hasimu ya kipa upande na mengine mengi.

Ni Kenya pekee ambapo tumeshuhudia Rais na Naibu wake wakitoleana maneno, yawe ya wazi au ya mafumbo, kuhusu hali ilivyo hasa nia ya Naibu Rais kutaka kuwania urais na makundi yake yanayomuunga mkono.

Ruto amekuwa akifanya ziara katika maeneo mbalimbali ya Kenya akitafuta kuungwa mkono huku akitoa misaada mbalimbali kama makanisani na makundi mengine, wakati mwingine akisaidiwa na ‘marafiki zake’; mambo ambayo Rais Kenyatta na wanaomuunga mkono wanayapuuza, wakisema hao wanatangatanga na wanahoji fedha hizo zinatoka wapi.

Pia, kumekuwapo na hatua kadhaa zinazochukuliwa na Serikali ya Rais Kenyatta kupambana na ufisadi, suala ambalo kundi la Ruto (kundi la Tangatanga” linaeleza kuwa hatua hizo zinawalenga wao na marafiki zao kwa lengo la kuwadhoofisha.

Hivi sasa kimeingia kivumbi cha kutaka katiba ya Kenya ifanyiwe marekebisho na kuingiza masuala kadhaa kama kubadili namba ya kuwapata mawaziri, maslahi ya viongozi wa watumishi na vuguvugu jipya la kushinikiza kubana matumizi yasiyo ya lazima ambalo limebatizwa jina la ‘Punguza Mzigo’.

Katiba ya Kenya iliandikwa upya mwaka 2010 na kuingizwa masuala ambalo baada ya mjadala mrefu yalionekana muhimu nchini humo, baada ya vurugu za kisiasa zilizotokana na uchaguzi wa mwaka 2007.

Hata hivyo, miaka tisa sasa imeanza kuonekana mianya ndani ya katiba hiyo iliyotajwa kuwa miongoni mwa zilizo bora barani Afrika, ambayo harakati zinafanyika kila mara kutaka kuziba, hasa zikiwa zinachagizwa na vuguvugu la uchaguzi wa 2022.

Mojawapo ya mkakati ni ule unaotajwa na Katiba ya Kenya ya 2010 katika Ibara ya 257 (4); kuwa mchakato wa mabadiliko ya Katiba unaweza kuanza ikiwa yataungwa mkono na wapiga kura angalau milioni moja nchini, ambalo limefanikiwa kwa hatua ya awali.

Punguza mzigo

Kampeni ya ‘Punguza Mzigo’ iliongozwa na chama cha Thirdway Alliance Kenya cha aliyekuwa mgombea urais Kenya, Ekuru Aukot.

Mpango huo unapendekeza mabadiliko ya mambo mbalimbali, ikiwamo kutaka muhula wa uraia uwe mmoja wa miaka saba badala ya mihula miwili ya miaka mitano kila mmoja, kadhalika unapendekeza kupunguza idadi ya wabunge na maseneta kutoka idadi iliyopo sasa ya 416 hadi 147.

Pendekezo la Punguza Mzigo likipitishwa, Wakenya watakuwa wamepunguza gharama ya kuendesha Bunge kutoka Sh36.8 bilioni hadi Sh5 bilioni kwa mwaka.

Hii inamaanisha kwamba, wataokoa Sh31.8 bilioni kwa mwaka ambazo zinaweza kutumi

iwa na zaidi ya watu milioni moja wanaotajwa na Katiba.

Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati amesema tume hiyo imeridhishwa na saini zilizowasilishwa, na safari ya kura ya maoni inaelekea katika serikali za kaunti 47 nchini.

“Wapigakura 1, 222, 541 waliotia saini kuiunga mkono. Hii ni kuuarifu umma na wadau wote kwamba mpango huo umefikia masharti yanayohitajika kwa mujibu wa katiba,” alisema Chebukati.

Hatua za maamuzi

Baada ya hatua hiyo, muswada ulioidhinishwa na IEBC Alhamisi, utawasilishwa kwa maspika wa mabunge 47 ya kaunti kuushughulikia ndani ya siku 30.

Kulingana na kipengee cha 257 (5), katika hatua hiyo, ikiwa utapitishwa na angalau mabunge 24 ya kaunti, muswada wa mchakato wa ‘Punguza Mzigo’ utawasilishwa katika Bunge la Kitaifa na Seneti.

Katika mabunge hayo mawili, mswada huo utashughulikiwa kwa kipindi cha siku 90, kama ilivyo miswada ya kawaida. Hii ina maana kuwa uamuzi wa Bunge la Kitaifa na Seneti utatolewa mwishoni mwa Machi 2020.

Uchambuzi wa Gazeti la Taifa Leo unabainisha kuwa endapo muswada huo utapitishwa na mabunge hayo kwa kura ya wengi, Rais Uhuru Kenyatta atautia saini na kuamuru uchapishwe kuwa sheria.

Kwa hivyo, hakutakuwa na haja na kuandaliwa kwa kura ya maamuzi ambayo inakadiriwa kuigharimu serikali angalau Sh15 bilioni.

Kura ya maamuzi

Lakini endapo muswada huo utakataliwa ama na Bunge la Kitaifa au na Seneti, muswada huo utawasilishwa kwa umma kuwa kura ya maamuzi ambayo itaendeshwa na IEBC.

Kulingana na kipengee cha 256 (5) cha Katiba tume hiyo itahitajika kuandaa kura hiyo ndani ya kipindi cha siku 90.

Ikiwa hilo litafanyika, ina maana kuwa shughuli hiyo itafanyika mwishoni mwa Juni 2020 baada ya kusomwa kwa Bajeti ya Kitaifa ya mwaka ujao wa kifedha wa 2020/2021.

Kulingana na kipengee cha 255, ibara ya (5) (a) na (b) muswada wa marekebisho ya katiba kwa njia ya kura ya maamuzi, sharti upate uungwaji mkono kutoka angalau asilimia 20 ya wapiga kura katika kaunti 24 au zaidi.

Muswada huu pia unaweza kuwa sheria ikiwa utapigiwa kuwa na wengi wa wapiga kura watakaoshiriki kura ya maamuzi.

Baada ya muswada huo kupitishwa katika kura ya maamuzi, mwenyekiti wa IEBC atauwasilisha kwa Rais Kenyatta, ndani ya siku 30 baada ya kukamilika kwa zoezi hilo.

Utachapishwa kuwa sheria baada ya kupata sahihi ya Rais.

Hata hivyo, wadadisi walionukuliwa na Taifa Leo wanasema muswada huo unatarajiwa kupata upinzani mkubwa katika Bunge la kitaifa, hasa miongoni mwa wabunge wa kike.

Hii ni kwa sababu unapendekeza kufutiliwa mbali kwa nyadhifa wabunge wawakilishi wa wanawake 47.

Vilevile, mchakato huo wa ‘Punguza Mzigo’ unataka kuondolewa kwa nafasi za wabunge na madiwani maalumu, wengi wao wakiwa wanawake na huenda watu fulani wakajaribu kuvuruga mpango huu kwa kuwasilisha kesi mahakamani kupinga uhalali wa IEBC.