Asali, mdalasini hutibu magonjwa lukuki

Tafiti mbalimbali za wataalamu wa lishe, zinaonyesha kwamba uwezo wa asali kutibu unaweza kuongezeka maradufu kama itachanganywa na mdalasini.

Asali inafahamika kama chakula muhimu kinachosaidia kupambana na magonjwa yatokanayo na uzee.

Tafiti mpya za wataalamu wa dawa lishe zimeonyesha kwamba asali inafahamika vyema duniani kama ‘silaha’ ya kiajabu katika kupigana na magonjwa mbalimbali.

Uchunguzi uliofanywa na jarida la World News kuhusu tiba, umeonyesha kuwa kuna umuhimu wa asali na mdalasini kuchanganywa pamoja.

Maumivu ya viungo vya mwili

Katika utafiti uliofanyiwa Chuo Kikuu huko Copenhagen, madaktari waliwapa wagonjwa 200 wa maumivu ya mwili, mchanganyiko wa kijiko kimoja cha asali na mdalasini kila asubuhi kabla ya kifungua kinywa.

Asilimia 73% ya wagonjwa hao walipata nafuu ya maumivu yao na ongezeko katika kufanya shughuli zao kama kawaida.

Kukatika kwa nywele

Asali ikishachanganywa na mdalasini pamoja na mafuta vuguvugu ya olive, hutoa kichocheo cha kuotesha nywele.

Mchanganyiko huo unapakwa kwa kusugua kichwani na kuachwa kwa dakika 15.

Ukungu wa miguuni (fangasi)

Kama una fangasi miguuni changanya kijiko kikubwa cha mezani cha asali, vijiko viwili vya mdalasini (vya chai), pakaa sehemu zilizoathirika usiku kwa muda wa nusu saa, kisha safisha kwa sabuni na maji.

Maambukizo kwenye kibofu cha mkojo

Chukua glasi ya maji ya vuguvugu yaliyochanganywa na vijiko viwili vya mdalasini na kijiko kimoja cha asali ili kuondoa bakteria kwenye kibofu. Kunywa mchanganyiko huu badala ya badala ya maji ikiwa ambukizo la kibofu linakuwa sugu.

Mchafuko wa tumbo

Asali imetambuliwa kwa kipindi kirefu kama dawa inayofaa kuondoa mchafuko wa tumbo pamoja na kichefuchefu.

Ongeza kiasi kidogo cha mdalasini na hii tiba ya maajabu vilevile itapunguza maumivu yaletwayo na vidonda vya tumbo.

Kula asali pamoja na mdalasini kunaweza kuondoa machafuko ya tumbo na utumbo uletwao na gesi kwa mujibu wa uchunguzi huko India na Japan.

Chunusi

Changanya vijiko vitatu vya asali pamoja na kijiko kimoja cha mdalasini na pakaa kwenye chunusi.

Uwezo wa asali wa kuua bakteria utaufanya uso wako kuwa kawaida katika muda wa wiki mbili.

Mwandishi wa makala haya ni mtaalamu wa tiba mbadala.