Ronaldo, Messi watoka uwanjani vichwa chini

Monday February 4 2019

 

Mabingwa wa Ligi Kuu Italia Juventus ‘Kibibi Kizee’ cha Turin, wamelazimishwa sare na Parma, baada ya kukosa nafasi nyingi za kufunga.

Juventus iliruhusu idadi kubwa ya mabao katika mchezo ambao timu hiyo ilikuwa nyumbani.

Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal, Gervinho aliyefunga mabao mawili, alipachika bao la kusawazisha dakika za majeruhi.

Ronaldo alifunga moja ya mabao katika mchezo ambao timu hizo zilitoka sare ya mabao 3-3.

Juventus ilikosa idadi kubwa ya mabao kwa kushindwa kutumia vyema nafasi walizopata ndani ya eneo la hatari la Parma.

Ronaldo amefikisha mabao 16 katika msimamo wa Ligi Kuu Italia akichuana katika mbio za kuwania kiatu cha dhahabu na Fabio Quagliarella wa Sampdoria.

Kigogo kingine cha soka Italia Barcelona, kililazimishwa sare ya mabao 2-2 na Valencia kwenye Uwanja wa Nou Camp.

Barcelona ilitoka nyuma na kusawazisha mabao hayo kupitia kwa nahodha Lionel Messi.

Mabao ya Kevin Gameiro na Dani Parejo yaliwashitua mabingwa hao wa Hispania kabla ya kuongeza kasi na kusawazisha.

Advertisement