Mtambue mtoto asiyepaswa kuajiriwa

Thursday April 4 2019

 

By Clavery Mlowe

Kwa mujibu wa sheria ya ajira na uhusiano kazini ya mwaka 2004, mtoto ni mtu mwenye chini ya miaka 14. Ni kosa kisheria kumwajiri mtoto wa chini ya wa umri huo.

Kwenye kazi hatarishi kwa mtoto, ni kosa kumwajiri mtu mwenye chini ya miaka 18 katika maeneo kama vile kazi za mgodini au vilabu vya pombe au zile za usiku.

Kanuni zinamkinga na kumlinda mtoto kujihusisha na ajira hatarishi na zisizo rasmi kwake.

Sheria inasema mtoto chini ya miaka 14 hapaswi kuajiriwa isipokuwa kufanya kazi nyepesi ambazo hazina madhara kwa afya yake na haziingiliani na mahudhirio yake shuleni.

Sheria inaagiza kutomzuia mtoto kuhudhuria masomo, kushiriki ufundi stadi au miradi ya mafunzo yaliothibitishwa.

Mtoto haruhusiwi kufanya kazi muda amabao anapaswa kuwa shuleni. kwa mtoto anayeendelea na masomo, haruhusiwi kufanyakazi kwa zaidi ya saa tatu kwa siku.

Advertisement

Mtoto mwenye miaka 14 au zaidi anapokuwa likizo, akihitimu elimu ya msingi au hasomi kwa sababu za msingi, anaweza kuajiriwa kufanya kazi kwa kipindi kisichozidi saa sita kwa siku na asiruhusuiwe kufanya kazi kwa saa tatu mfululizo bila kupumzika walau kwa saa moja.

Sheria piainabainisha kuwa umri wa chini kwa kazi hatarishi ni miaka 18. Mtu yeyote haruhusiwi kumwajiri mtoto kwenye ajira inayohatarisha ustawi wake, inayotishia elimu, afya ya mwili na akili au maadili yake.

Mtu anaye anayemtumikisha mtoto anafanya kosa na akithibitika anaweza kupata adhabu ya kulipa faini ya Sh100,000 au kifungo cha miezi mitatu au vyote viwili kwa pamoja.

Ni kinyume na sheria kwa mtu yeyote kuajiri mtoto katika kazi hatarishi inayoweza kusababisha athari za kiafya, usalama au maadili.

Kazi hatarishi ni pamoja na vyombo vya majini, kubeba mizigo mizito, kazi za viwadani kunazotumika au kuzalishwa kemikali, kazi zinazotumia mashine na kazi za usiku kati ya saa 12:00 jioni na saa 2:00 usiku.

Mtu yeyote anayeona mtoto akishiriki kazi hatarishi anapaswa kuchukua hatua kuzuia hali hiyo. Kumzuia mtoto kwenda shule kutokana na kazi anazopewa ni kosa sheria.

Advertisement