Faida za kuku katika ufugaji mseto wa samaki

Muktasari:

Hiki huwapa samaki afya nzuri kwani huwa na chembechembe nyingi za urea ambazo ni sehemu kubwa ya madini ya Nitrojeni na Fosforasi ambayo huhitajika kwa wingi kwenye chakula cha samaki.

Lengo kuu la ufugaji wa kuku kwenye ufugaji mseto ni urutubishaji wa bwawa la samaki ili kupata chakula cha asili kwa samaki. Kinyesi cha kuku hutumika kama chanzo cha mbolea kwa sababu huwa kina kiasi kikubwa cha urea.
Mbili, hutoa chakula cha samaki. Tofauti na kuwa chanzo cha rutuba, kinyesi cha kuku huliwa moja kwa moja na samaki.

Hiki huwapa samaki afya nzuri kwani huwa na chembechembe nyingi za urea ambazo ni sehemu kubwa ya madini ya Nitrojeni na Fosforasi ambayo huhitajika kwa wingi kwenye chakula cha samaki.
Tatu, chanzo cha chakula kwa wafugaji. Pamoja na kuwa na umuhimu wa kiikolojia katika ufugaji mseto, lengo jingine kubwa ni kuwa chanzo cha lishe bora kwa mfugaji kwani huwa na protini ya kutosha ambayo husaidia katika ukuaji wa mwili.
Nne, chanzo cha fedha. Kama ilivyo kwa mifugo wengine, mauzo yatokanayo na mazao kama kuku husaidia kama chanzo kikubwa cha fedha kuanzia wafugaji wadogo wadogo hadi wakubwa.
Kuku hufugwa kirahisi kulinganisha na wanyama wakubwa kama vile ng’ombe, nguruwe, mbuzi na kondoo ambao huhitaji eneo kubwa, rasilimali kubwa, wasimamizi wengi, n.k. Hivyo ufugaji wa kuku huwa na gharama ndogo kiuendeshaji na huleta faida kubwa.