Mshambuliaji mpya wa Azam, Mbaraka agoma kuzungumzia mkataba wa Kagera Sugar

Tuesday June 13 2017

 

By [email protected]

Dar es Salaam. Mshambuliaji mpya wa Azam, Mbaraka Yusuph amesema hawezi kuzungumzia taarifa zinazoenea kuwa bado ana mkataba mpya na Kagera Sugar.

Akizungumza na mtandao huu, mshambuliaji huyo aliyefunga mabao 12 msimu uliopita alisema kwa sasa anapumzika akijiandaa na majukumu ya kitumikia timu yake mpya msimu ujao.

“Suala hilo, siwezi kulizungumzia, kila mtu ataongea lake,”alisema kwa ufupi.

Mratibu wa Kagera Sugar, Mohammed Hussein hakupatikana kutolea ufafanuzi kuhusu taarifa hizi kwa kuwa muda wote simu yake iliita bila kupokewa.

Advertisement