Neno la Padri ibada ya kuagwa Akwilina

Muktasari:

Padri Lyimo ametoa kauli hiyo leo Februari 23, 2018 katika Kanisa la Mtakatifu Theresia Parokia ya Olele Rombo mkoani Kilimanjaro katika ibada ya kuaga mwili wa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwiline.

 Mwakilishi wa Askofu Isaac Amani wa Jimbo Kuu la Arusha, Padri Emmanuel Lyimo amewataka wananchi kutumia vipawa walivyopewa na Mungu kutenda mema.

Padri Lyimo ametoa kauli hiyo leo Februari 23, 2018 katika Kanisa la Mtakatifu Theresia Parokia ya Olele Rombo mkoani Kilimanjaro katika ibada ya kuaga mwili wa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwiline.

"Wanadamu tumeumbwa na kukirimiwa vipawa viwili; ambavyo ni akili na utashi. Vipawa hivi tuvitumie kama Mwenyezi Mungu anavyotaka,” amesema Padri Lyimo na kuongeza:

 "Akili ituongoze kuchagua na kufikiri yaliyo mema. Mwanadamu akitenda kinyume na Mungu aliyemkirimisha hivyo anatenda dhambi,"

Amesema iwapo  mwanadamu atatenda dhambi hiyo, anajiweka katika mazingira hatarishi ya kutomuona Mungu milele.

Ibada hiyo imemalizika saa 7:46 mchana na sasa waombolezaji wanaelekea nyumbani kwa wazazi wa mwanafunzi huyo kwa ajili ya kupumzisha mwili wa Akwilina katika nyumba yake ya milele.